RUVU SHOOTING YAPANIA KUTWAA KOMBE LA MAADHIMISHO YA MIAKA 50 YA JWTZ

TIMU ya Ruvu Shooting ya Mlandizi Pwani imejitapa kutwaa ubingwa wa michuano maalum ya soka ya kuadhimisha miaka 50 tangu kuanzishwa kwa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) inayotarajiwa kuanza Julai 4 hadi 7 katika viwanja vya Bandari jijini Dar es Salaam. 
Tayari kikosi cha wachezaji 18 na viongozi watano wa maafande hao wameshawasili jijini Dar es Salaam kwa ajili ya mashindano hayo yatakayoshirikisha michezo mbalimbali ikiwemo soka itakayoshirikisha timu saba zikiwemo , Ruvu Shooting, JKT Oljoro, Mgambo Shooting, JKT Ruvu, Kanembwa JKT na  Mlale JKT
 Msemaji wa Ruvu Shooting Masau Bwire ameiambia Sports Lady Blog  kwamba,wamejipanga vema kushiriki michuano hiyo na hatimaye kutwaa ubingwa. 
“Tupo tayari kwa ajili ya kushiriki michuano hii kikamilifu ili kushinda na kudhihirisha kwamba sisi ni moja ya timu bora kati ya zile za majeshi hapa nchini,”alisema 

Bwire aliongeza kuwa, kupitia michuano hiyo wanatarajiwa kushusha jeshi la wachezaji wote wakali ikiwemo wapya ambao wamesajiliwa hivi karibuni kwa ajili ya kukiimarisha kikosi hicho kwenye ligi kuu bara msimu wa 2013/2014.