RAIS KIKWETE KUWA MWAMUZI WA MTANANGE KATI YA WABUNGE WA YANGA NA SIMBA

Rais Dk. Jakaya Mrisho Kikwete.
Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Jakaya Mrisho Kikwete, amekubali kuwa mgeni rasmi katika Tamasha la Usiku wa Matumaini litakalo fanyika Jumapili hii, Julai 7 katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam. Aidha, Rais atahutubia katika tamasha na pia atakuwa refa wa mechi za wabunge wa Yanga na Simba.