NICO NYAGAWA AREJESHEWA ULAJI WAKE SIMBA SC

KLABU ya Simba imemrejesha kundini nahodha wake wa zamani Nico Menard Nyagawa (pichani)ambaye atakuwa meneja ndani ya timu hiyo hiyo.Sports Lady Blog inakujuza.
Awali Nyagawa ambaye baada ya kustaafu alikuwa akitumika katika nafasi hiyo kabla ya kuondolewa ‘kimizengwe’ na nafasi kuchukuliwa na kocha Moses Basena.
Taarifa zinaeleza kwamba, Basena pamoja na Jamhuri Kihwelo ‘Julio’ watakuwa wakimsaidia kocha mkuu Abdallah ‘king’ Kibaden katika kukinoa kikosi cha timu hiyo.

Simba inaendelea na mazoezi yake katika uwanja wa Kinesi kwa ajili ya kujiandaa na michuano mbalimbali pamoja na Ligi Kuu Bara.