MTIHANI WA KWANZA KWA MNIGERIA WA YANGA UWANJA WA TAIFA J'2

MTIHANI wa kwanza kwa mshambuliaji wa kimataifa wa Yanga,  Mnigeria Ogbu Brendan utakuwa jumapili ya keshokutwa pale atakapoichezea timu yake dhidi ya URA.
Yanga na URA zitakwaana siku hiyo katika mchezo wa kimataifa wa kirafiki utakaofanyika kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Brendan aliyetua nchini mapema wiki hii kwa ajili ya kufanya majaribio na klabu hiyo, hiyo itakuwa mechi yake ya kwanza na timu hiyo akiwaniwa kusajiliwa.

Kwa sasa Yanga ambao ni mabingwa wa Ligi Kuu soka Tanzania Bara wapo katika mchakato wa kusaka mshambuliaji ambaye atashirikiana kwa karibu na Didier Kavumbagu.