MISS UTALII TANZANIA KUONGOZA WAREMBO NA WANAMITINDO TANZANIA KATIKAMBIO MBIO ZA NYIKA ZA KUPIGA VITA UJANGILI

Mshindi wa Taji la Taifa la Miss Utalii Tanzania 2013, Hadija Saidi ambaye pia ni Miss Utalii Morogoro 2012/13, sambamba na washindi wa Taifa na Dunia wa Miss Utalii Tanzania, wataongoza warembo na washindi wa mashindano yote ya urembo nchini na nchi jirani, katika mbio za nyika za kimataifa za Ant Poaching International Marathon, National Parks International Marathon na Wildlife International Marathon 2013, zitakazo fanyika wakati wa Tamasha la kimataifa la Safari Kuu ya Utalii Tanzania la "Tanzania Great Safari Tour ' 2013, litakalo fanyika kuanzia mwezi Agosti hadi Septemba mwaka huu , katika Ukanda wa Kaskazini, Kusini,Mashariki na Magharibi wa Utalii.
Mbio hizo za kimataifa za Nyika za ANT POACHING MARATHON 2013, NATIONAL PARK MARATHON 2013 na WILDLIFE MARATHON 2013 ni sehemu ya Tamasha la kimataifa la SAFARI KUU YA KITALII TANZANIA 2013 yaani "TANZANIA GREAT SAFARI TOUR 2013" ambalo pamoja na malengo mengine linalenga katika kuhamasisha vita dhidi ya Ujangili ikiwemo Uwindaji Haramu, Uvunaji Haramu wa maliasili za Misitu na Baharini ikiwa ni pamoja na Uvuvi haramu na Uharibifu wa Mazingira. Ujangili limekuwa ni janga la kitaifa na tishio kubwa la Ustawi na ukuaji wa Utalii nchini na Duniani, ambapo hatua na juhudi za pamoja zisipochukuliwa sasa basi wanyama waliopo katika hifadhi za Taifa na Mapori ya akiba watatoweka na kuziacha hifadhi hizo zikiwa hazina wanyama tena hasa Tembo,Vifaru,Twiga na jamii nyingi za wanya ambazo hutumika kama kitoweo kwa binadamu.
Upo ujangili wa uvunaji na usafirishaji haramu wa Misitu ambayo hutoa  magogo na mbao, na kuliacha Taifa likipoteza mapato ,huku uvunaji huo haramu ukitishia maeneo ya misitu hiyo kuwa jangwa. Ujangili ukiachiwa utakosesha watoto wetu na vizazi vijavyo Urithi wa Taifa, lakini pia Taifa litapoteza Mapato yatokanayo na Utalii na Uvunaji mwingine wa Maliasili za nchi. Ujangili ni uhujumu uchumi, kwani sekta ya Utalii inachangia zaidi ya 17% ya Pato la Taifa kila mwaka, zaidi ya 25% ya pato la fedha za kigeni la Taifa na zaidi ya 12% ya ajira zote nchini na Duniani.
Tamasha la "Tanzania Great Safari Tour 2013, nisafari kuu ya kitalii, ambayo itawajumuisha na kuwaweka pamoja Waandishi wa Habari, Vyombo Vya Habari vya TV,Redio,Magazeti, Majarida, Mitandao ya Internet, Mitandao ya Kijamii na Tovuti. Warembo,Wanamitindo,Wanamichezo, Wana Muziki na Wasanii wa Ngoma za Asili na Filamu, wakitembelea Hifadhi za Taifa ,Ngorongoro Crater, Mapori ya Akiba, Hifadhi za Bahari, Maeneo ya Kitamaduni na Kihistoria huku wakipiga picha za vyombo vya habari vya kitaifa na kimataifa vya Televisheni, Filamu,Video ,Minato, Matangazo ,Makala, Promo DVD'S ,Vipindi vya Televisheni na Majarida huku wakihamasisha Utalii wa Ndani, Vita Dhidi ya Uwindaji Haramu, Uvuvi Haramu, Ujangili na Uharibifu wa Mazingira, huku pia wakitangaza Vivutio vya Utalii Vya Tanzania kitaifa na kimataifa.
Mbali ya washiriki wa kitaifa , pia kutakuwa na washiriki wa kimataifa, wanadiplomasia, Viongozi wa Serikali, Mashirika ya Kimataifa, Umma, Binafsi na Washiriki binafsi ambao wataandikishwa au watakao hamasika kushiriki. Tamasha la "Tanzania Great Safari Tour 2013 ni Tafsiri vitendo ya Sera ya Taifa ya Utalii, Wanyama Pori, Misitu, Utamaduni ,Uvuvi na Mazingira. Hii itakuwa ni fulsa nyingine kwa Tanzania na mamlaka zake za Utalii sio kutangaza Vivutio vya Utalii Tuu bali kupiga vita Ujangili hususani uwindaji haramu kitaifa na kimataifa. Aidha hii itakuwa ni fulsa kwa Makampuni, Mashirika, Asasi za Umma na binafsi kujitangaza kupitia Tamasha hili kwani litarushwa moja kwa moja (LIVE) katika Televisheni na Internet , na kuangaliwa na zaidi ya watazamaji 680 Milioni Duniani kote. Tamasha hili linaandaliwa na Africa Tourism Promoshen Centre kwa kushirikiana na Miss Tourism Tanzania Organisation.
Asante,
Erasto Chipungahelo
Mwenyekiti Mtendaji – AfricaTourism Promotion Centre / Miss Tourism Tanzania Orgaisatio

Comments