MABONDIA KIBAO KUZICHAPA SIKU YA IDD FRIENDS CORNER HOTEL

baadhi ya vijana wa bigright wakiwa mazoezini
Kipindi cha hivi karibuni tumeona Mabondia wa zamani,wadau wa karibu wa ngumi na makocha wa mchezo huo wameamua kuzikomalia ngumi wenyewe kwa kuwaandalia mabondia wao mapambano mbalimbali yakiwemo mapambano yatakayofanyika siku ya idd katika kumbi mbalimbali kama vile friends corner hotel – manzese,idi bonge na bahati mwafiale watazipiga id mosi nasibu ramadhan na juma fundi idi pili . CCM hall kiwangwa mabondia wa chalinze watacheza na wa kiwangwa, eagle bar bagamoyo bingwa wa zamani wa kickboxer wilayani pwani tomb po ambae ni mwanafunzi wa japhet kaseba atazipiga na Daud Anthony’odinga’toka kambi ya bigright boxing.katika mapambano ya bagamoyo yameandaliwa na Tan academy ya kaseba akishirikiana bigright promotion inayosimamiwa na Ibrahim kamwe.
Mkoani songea katika uwanja wa majimaji musa omar chitepete atazipiga na obote ameme wakati iringa roy mbunda atazipiga yusuf jibaba.na mapambano mengineyo mengi tu tandika,mwananyamala,morogoro nakadhalika kote ngumi zimeandaliwa kufanyika siku hiyo ya idi katika kuuboresha,kunyanyua vipaji na kutoa burudani kwa wapenzi wa mchezo huo  wa ngumi nchini lakini cha kusikitisha na kinachokatisha tama sehemu zote hizo zilizotajwa hakuna hata moja iliyopata udhamini au ufadhili wa kueleweka kuendesha mapambano hayo ,yatajiendesha kiubishiubishi kwa kutumia uzoefu mdogo wa mabondia wa zamani,makocha na wadau wachache wachovu kufanikisha mapambano hayo.
Hii ukitoa lile pambano la dar live la francis miyeyusho na fidelis toka Zambia.