KIGGI KWENDA KUTIBIWA INDIA,SIMBA KUADHIMISHA WIKI YA JAMII AGOSTI 5 HADI 11                        Simba Sports Club inatarajia kuwa na wiki ya kijamii kuanzia tarehe 5/8/2013 hadi tarehe 11/8/2013 na programu itakuwa kama ifuatavyo:-
5/8-KUTEMBELEA KITUO CHA WATOTO YATIMA NA KUTOA MSAADA
6/8-KUTEMBELEA WAGONJWA WASIOJIWEZA HOSPITALI NA KUTOA MSAADA
7/8-KUHUDHURIA KOZI/SEMINA ILIYOANDALIWA NA WADHAMINI TBL PAMOJA NA KUTEMBELEA KIWANDA CHA TBL
8/8-SIMBA DAY
9/8-KUTEMBELEA SHULE YA MSINGI NA KUHAMASISHA MICHEZO MASHULENI
10/8-KUTEMBELEA MEDIA HOUSE ILI KUENDELEZA MAHUSIANO MEMA NA VYOMBO VYA HABARI
11/8-KUFANYA DUA NA IBADA KLABU KATIKA IMANI ZOTE (KUWAOMBEA REHEMA WALIOTANGULIA, KUOMBA MEMA KATIKA MSIMU UJAO).


MAENDELEO YA MPANGO MKAKATI WA KLABU (STRATEGIC PLAN)
 Open university wameishatuma draft ya kwanza ya Strategic Plan ambapo Kamati ya Utendaji mnamo tarehe 13/7/2013 itakutana na kamati ya marejeo kuipitia strategic plan hiyo ili kuijadili kwa mapana kurudisha mrejesho kwa ajili ya kuandaa draft ya mwisho tayari kuingizwa Mkutano Mkuu wa wanachama.


SUALA LA MATIBABU YA KIGI MAKASI
 Timu ya kitabibu ya Simba Sports Club ipo katika mchakato wa kupata “appointment” nchini India kwa ajili ya kumsafirisha KIGI MAKASI kupata matibabu zaidi nchini humo baada ya kupata rejesho la daktari wa timu. Mchezaji husika anatarajiwa kuwa nchini India mwanzoni mwa mwezi ujao.


IMETOLEWA NA

EZEKIEL KAMWAGA
AFISA HABARI
SIMBA SPORTS CLUB
4/7/2013