FAINALI AIRTEL RISING STARS KURUSHWA 'LIVE' SUPER SPORT


Fainali za michuano ya Airtel Rising Stars kwa wavulana na wasichana zinazochezwa kesho (Julai 6 mwaka huu) Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume, Dar es Salaam zitaoneshwa moja kwa moja na kituo cha televisheni cha SuperSport.
  1. Mechi za fainali ambazo mgeni rasmi atakuwa Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Amos Makala zitachezwa kuanzia saa 7.30 mchana kwa wasichana wakati ile ya wavulana itaanza saa 9.30 alasiri.

Nusu fainali za mashindano hayo ambazo pia zinaonekana moja kwa moja SuperSport zinachezwa leo (Julai 5 mwaka huu). Kwa upande wa wasichana ni kati ya timu za Kinondoni na Kigoma wakati Ilala inaumana na Temeke.
Kwa upande wa wavulana nusu fainali ya kwanza ni kati ya Mwanza na Ilala ambapo baadaye itafuatiwa na nyingine kati ya Morogoro na Kinondoni. Mechi za kutafuta mshindi wa tatu zitachezwa kesho asubuhi (Julai 6 mwaka huu).


Comments