COASTAL UNION YAMKANA KASEJA, YASEMA HANA NAFASI

KLABU ya soka Coastal Union ya Tanga ‘Wagosi wa Kaya’ imevunja ukimya na kukana kumsajili ama kuwa na mpango wa kumsajili aliyekuwa kipa wa Simba, Juma Kaseja.
Mkurugenzi wa Ufundi wa Coastal Union, Nassor  Bin Slum amesema  kwamba Kaseja hana nafasi ndani ya klabu hiyo kutokana na ukweli kwamba tayari wana makipa watatu wanaoweza kukidhi mahitaji ya klabu hiyo.
“sisi tunasajili kwa mipango na hatuangalii majina kwani katika safu ya makipa tuna  Said Lubawa tuliyemsajili toka JKT Oljoro,yupo Shaban Kado, pia tunaye Mansoor Mansoor ambaye tumempandisha kutoka timu  B,”alisema
Bin Slum aliongeza kwamba watu walijenga imani kuwa  timu yao itakuwa sebule ya wachezaji waliotemwa Simba baada ya kusajali Haruna Moshi ‘Boban’ na Juma Nyoso, lakini ukweli ni kwamba nyota hao walisajiliwa kutokana nas ytimu yao kuhitasji wachezasji wa nafasi hizo.

“Baada ya kuwanyakua Bonas nas Nyoso mengine yakazushwa mara tunamsajili redondo (Ramadhan Chombo), mara Amir Maftah yote sijui yalitoka wapi, sisi tunasajili kwa malewngo maalum,”aliongeza.