BOBAN, NYOSO KUTAMBULISHWA MKWAKWANI J'5 DHIDI YA URA

                                                                                 BOBAN
KLABU ya Coastal Union ya Tanga siku ya jumatano inatarajiwa kuwatambulisha rasmi wachezaji wake wapya iliowasajili kwa ajili ya msimu mpya wa Ligi Kuu Bara ,kupitia mchezo wa kimtaifa wa kirafiki dhidi ya URA ya Uganda utakaopigwa kwenye dimba la Mkwawani mjini Tanga.

Coastal ambayo kwa sasa inaendelea na mazoiezi ya kujiandaa na ligi hiyo inayotarajiwa kuanza Agosti 24 mwaka huu, imewasajili wachezaji kadhaa kwa ajili ya kuimarisha kikosi chake kwenye ligi hiyo wakiwemo nyota waliotoka klabu ya Simba, Haruna Moshi 'Boban' na Juma Nyoso.
Mratibu wa mchezo huo, George Wakuganda amesema kwamba maandalizi ya mchezo huo yanaendelea vema na kuwataka mashabiki kujitokeza kwa wingi siku ya mechi hiyo.
URA ipo nchini kwa ziara ya kimichezo ambapo jumamosi ilikipiga na Simba na kushinda mabao 2-1 kabla ya jana kutoka sare ya 2-2 dhidi ya Yanga katika michezo iliyopigwa Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.