VODACOM YAITAKIA KILA LA HERI STARS JUMAPILI

Dar es Salaam, Juni 13, 2013 …Mdhamini Mkuu wa ligi kuu ya Tanzania Bara, Kampuni ya Mawasiliano ya Simu ya Vodacom Tanzania imetoa wito kwa mashabiki wa soka nchini kujitokeza kwa wingi na kuishangilia timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars siku ya jumapili itakapomenyanya na timu ya taifa ya  Ivory Coast.
Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania , Rene Meza amesema kuwa Taifa Stars bado inabea matumaini makubwa kwa Tanzania kushiriki kwa mara ya kwanza katika fainali za kombe la dunia zitakazofanyika mwakani nchini Brazil
“Hakuna ubishi kwamba katika soka lolote huweza kutokea lakini kwa Taifa Stars hesabu za soka bado zinatoa nafasi kusonga mbele bila hata kuhitaji miujiza ya soka., kikubwa na taifa kuendelea kuamini katika kikosi cha Stars na Mwalimu Poulsen(Kim)”Alisema Meza
“Wananchi wamekuwa nyuma ya Stars kwa wakati wote na ni Imani yangu kwamba tutanedelea kufanya hivyo kwa mechi ya Jumapili dhidi ya Ivory Coast, ni timu yenye jina kubwa Barani Afrika lakini hilo halizuii uwezo mkubwa wa kikosi cha Stars cha sasa.”
“ Meza amesema kuwa katika kuhakikisha kuwa idadi ya mashabiki inaongezeka siku hiyo ya mpambano huo wa Stars dhidi ya Tembo wa Ivory Coast, Vodacom Tanzania imeweka mpango maalumu na kuwafaidisha wateja wanaotumia mtandao wa simu za Vodacom ambapo watapata tiketi za VIP kama njia ya kuhamasisha kuishabikia timu ya Taifa Stars.
“Tumetengeneza mpango maalum wa kuwahamasisha Watanzania wenye uzalendo na kuishabikia timu yetu ya Taifa kwa moyo mmoja. Tumeamua kuweka nafasi hiyo kama motisha kwa mashabiki wa soka kwa kujipatia tiketi za bure kwenda kuangalia mechi hiyo, Mteja wa Vodacom atatuma neon TAIFA kwenda 15577 na atapata wimbo wa kuhamasisha ushindi wa taifa Stars na nafasi ya kujishindia tiketi za VIP,”alisema Meza.
Aidha  Meza ambae amekuwa muumini mzuri wa maendeleo ya soka la Tanzania kwa kuweka mazingira bora yanayowezesha kuwepo kwa ushindani wa hali ya juu katika ligi kuu kupitia udhamini wa Vodacom hatua inayosaidia kupatikana kwa kikosi bora cha timu ya taifa, amesema kuwa hamasa ya ushindi kwa timu hiyo ya Taifa Stars ni kubwa kwa wachezaji, mwalimu na taifa kwa ujumla.
“Vodacom Tanzania tunatambua umuhimu wa mchezo huo na tunaungana na watanzania na wadu wote wa soka kuitakia kila la heri timu ya taifa katika mchezo wao wa Jumapili.”Aliongeza Meza wakati akitoa maoni yake kuelekea mchezo huo unaotazamiwa kuandika historia mpya ya soka la Tanzania ndani na katika uso wa kimataifa
Timu ya Ivory Coast inatarajiwa kutua leo nchini kwa ndege maalum ikiwa na msafara wa jumla ya watu 80 na kufikia kwenye  hoteli ya Bahari Beach iliyopo nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam.