UCHAGUZI WA VIONGOZI WA SHIRIKISHO LA NDONDI UPO PALE PALE

    
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Yah:- Uchaguzi wa viongozi wa BFT.

Uchaguzi wa viongozi wa BFT uliopangwa Kufanyika tarehe 7/7/2013 jijini Mwanza, utafanyika kwa tarehe hiyo kama ulivyopangwa.
Kikao cha kamati ya utendaji ya BFT kilichofanyika juzi katika  ofisi za BFT kikiongozwa na Rais wa shirikisho Joan Minja kimesisitiza kuwa uchaguzi utafanyika kama ulivyopangwa na haujaairishwa kama baadhi ya kikundi cha watu wachache wanaojiita wadau wanavyoweka pingamizi na  kupotosha  kwa kuwashawishi wajumbe wa mkutanao mkuu hasa kutoka mikoani kutohudhuria mkutano huo wa uchaguzi,kwa manufaa yao binafsi na kinyume na katiba yetu.
Upotoshaji huo unafanywa na  Akaroly Godfrey aliyekuwa  kiongozi katika uongozi uliojiudhuru kutokana na kashfa za kusafirisha madawa ya kulevya na kusababisha Tanzania kufutwa uanachama na chama cha ngumi cha dunia (AIBA) na kusababisha  kutoshiriki mashindano,mikutano na shughuri zote za kimataifa za chama cha ngumi cha Dunia AIBA. Naomba wadau na serikali kuwa makini na watu wanaoshawishi kwa lengo la masilahi yao binafsi na kusababisha michezo kudolola badala ya kusonga mbele.
Fomu za uchaguzi zilishaanza kutolewa na Baraza la Michezo la Taifa (BMT) toka tarehe 4//2013 na zitaendelea kutolewa hadi tarehe 4/7/2013 jijini Mwanza na tarehe hiyo  ndio itakuwa siku ya mwisho ya kuchukua na kurudisha fomu, tarehe 5/7/2013 itatakuwa siku ya usaili na utafanyika jijini mwanza, tarehe 6/7/2013 kupitia pingamizi na kuzitolea maamuzi na tarehe 7/7/2013 ndio siku ya uchaguzi.
Kimsingi taratibu zote za kuitisha uchaguzi kwa mujibu wa katiba yetu zimezingatiwa na zimekamilika.
Aidha BFT inatoa tamko kwa wajumbe wa Mkutano Mkuu kufika katika uchaguzi uchaguzi, ili kupata viongozi halali kwa mujibu wa katiba, waendelee na shughuri za kuendeleza mchezo wa ndondi na kuaandaa timu ya taifa kushiriki katika mashindano ya Afrika nchini Mauritius Sept. 2013.
BFT inatoa wito kwa watu wote wenye sifa, nia, moyo na uwezo wa kuongoza wajitokeze kuchukua fomu za kugombea uongozi kwani wakati ndio huu. 
 
Makore Mashaga
Katibu Mkuu.


Comments