TWANGA PEPETA KUPAMBA SHINDANO LA MISS SINZA IJUMAA HII @ MEEDA CLUB

 Redds Miss Sinza ambaye pia ni Redds Miss Tanzania, Brigitte Alfred  alisisitiza jambo kwa warembo wa Redds Miss Sinza 2013  alipotembelea kambi ya mazoezi hiyo. Warembo hao watapanda jukwaani Ijumaa kuwania taji la mwaka huu. (Picha/Mpiga picha wetu).

Na Mwandishi Wetu
BENDI yenye chati ya juu kabisa katika muziki wa dansi nchini,  The African Stars’ Wana Twanga Pepeta’ itaburudisha mashindano ya Redds Miss Sinza yaliyopangwa kufanyika Ijumaa (Juni 7) kwenye ukumbi wa Meeda Club wa Sinza jijini.
Mratibu wa mashindano hayo, Majuto Omary alisema kuwa bendi hiyo itatumia fursa hiyo kutambulisha baadhi ya nyimbo zake mpya zilizomo katika albamu ya 12 ijulikanayo kwa jina la Nyumbani ni Nyumbani ambayo itazinduliwa rasmi Juni 30 kwenye viwanja vya Leaders Club jijini.
Majuto alisema kuwa Twanga Pepeta itakuwa ikitumbuiza kwa mara ya kwanza tokea mwaka jana mwezi  julai ambapo ilitumbuiza katika mashindani hayo hayo ya kumsaka mrembo wa Sinza. Alisema kuwa hii ni faraja kubwa kwa mashabiki wa muziki wa dansi na wa masuala ya urembo kwani Twanga Pepeta itakuwa ikimvua taji Redds Miss Tanzania, Brigitte Alfred ambaye atakuwa anavua taji lake la kwanza.
“Ikukmbukwe kuwa twanga pepeta haijatumbuiza Sinza kwa kipindi kirefu na hivyo kuandaa zawadi maalum kwa mashabiki wake katika mashindano hayo yaliyo dhaminiwa na Redds Original, Dodoma Wine, Chilly Willy Energy Drink, Fredito Entertainment, CXC Africa, Clouds Media Group, Salut5.com na Sufiani Mafoto blog,” alisema Majuto.
Alisema kuwa jumla ya warembo 12 wamejitokeza kuwania taji la mwaka huu la Sinza nan i matarajio ya waandaaji kuwa Miss Sinza wa mwaka huu atatwaa taji hilo na kufuata nyayo za Brigitte ambaye aliweza kutwaa taji la Miss Kinondoni na baadaye Miss Tanzania.
“Tuna warembo bora ambayo wamedhamilia kufanya kweli katika mashindano ya urembo mwaka huu,  wamepania kulinda hadhi ya mwaka jana, hivyo mashabiki waje kuona warembo bora waliopania kufanya kweli katika mashindano hayo,” alisema.

Comments