SUNZU APEWA MKONO WA KWA HERI SIMBA SC

HABARI ndiyo hiyo!licha ya kumaliza mkataba wake na klabu ya Simba, mshambuliajia wa kimtaifa Mzambia Felix Sunzu hana nafasi tena ya kusajiliwa  katika klavbu hiyo.
Sunzu aliyejiunga na Simba mwaka juzi amekuwa akiumiza vichwa vya viongozi wa timu hiyo  ambao walishindwa kuvunja mkataba wake mnono baada ya kushindwa kuitumikia ipasavyo licha ya kulipwa pesa nyingi.
Hiyo ilitokana na kuhofia kutoa fedha nyingi kama wangevunja mkata hivyo ilibidi kuwa na subira mpaka amalize mkataba.
Aidha kocha msaidizi wa Simba, jamhuri Kihwelo 'Julio' naye amepigilia nyundo juu ya nyota huyo na kusema kuwa hawamuhitaji katika kikosi chake.
Bila ya kupepesa mdomo Julio ameiambia Sports Lady Blog hii leo kwamba, hawaoni umuhimu wa Sunzu kurejeshwa tena Simba kwani kwa nafasi yake kuna wachezaji wengi wazuri zaidi yake.
"Sassa hivi kikosi chetu ni kizuri sana na hata hilo pengo la Sunzu halipo, hana nafasi kabisa katika kikosi chetu kwani kuna vijana wazuri kuliko yeye",alisema Julio
Tayari kocha mkuu wa Simba Abdallah 'king'kibaden naye alishasema haoni umuhimu wa wachezaji wa kigeni ndani ya klabu hiyo kwani hapa nchini kuna wachezaji wengi wazuri zaidi yao.