Mwakilishi wa kampuni ya Steps Solar, Johnson Mwamba (mwenye
koti) akizungumzia udhamini wa kampuni yao
katika tuzo za Steps Movie Award zilizopangwakufanyika Jumamosi kwenye ukumbi
wa Blue Pearl.
Meneja Masoko wa Steps Entertainment, Kambarage Ignnatus
akionyesha moja ya tuzo zitakaotolewa kwa wasanii sikuya Jumamosi kwenye ukumbi
wa Blue Pearl, Ubungo
Plaza , kulia ni Mwakilishi wa kampuni ya Steps Solar, Johnson
Mwamba.
Na Mwandishi Wetu
Kampuni ya usambazaji wa filamu Tanzania
ya Steps Entertainment limited Jumamosi
itatoa tuzo kwa wasanii, Watayarishaji, Waongozaji, na wadau mbalimbali
waliopo katika tasnia ya filamu Tanzania .
Mratibu wa tuzo hizo, Carlos Johns Silondwa alisema kuwa
tuzo hizo zitafanyika kwenye ukumbi wa Blue
Pearl Ubungo
Plaza na zitawahusisha zaidi wasanii
wanaofanya kazi na kampuni yao
tu.
Silondwa alisema kuwa kutakuwa na vipengele nane ikiwa
pamoja na Filamu Bora ya Mwaka, Kampuni iliyotengeneza filabu bora, msanii
anayependwa na watu ndani na nje ya mwisho, msanii bora chipukizi, muigizaji
bora wa kike, muigizaji bora wa kiume, muongozaji bora wa filamu na mwandishi
bora wa filamu.
Silondwa alisema kuwa wameandaa tuzo hizo kwa lengo la
kuanzisha tuzo hizo ni kuleta ushindani na kukubali mchango wa wasanii,
watayarishaji na wadau wote kampuni inatumia fursa hii ya kuwatambua na kujali
mchango wa wasanii katika ukuzaji wa filamu nchini Tuzo ni kichocheo kitakacholeta
ushindani unaoweza kujenga tasnia ya filamu na kujenga ajira kwa jamii kubwa.
Alisema kuwa tuzo hizo zimezingatia michango mbalimbali
kutoka kwa wadau mbalimbali ambao wamekuwa mbele katika kutangaza tasnia ya
filamu ndani na nje ya nchi kupitia njia mbalimbali, pia kutakuwa na tuzo za
heshima kwa waliotangulia kuitambulisha tasnia ya filam u Tanzania .
“Tunaamini kuwa tuzo zitakuwa kichocheo kikubwa cha kukuza
tasnia ya filamu kuongeza ushindani katika kutengeneza filamu Bora, hadithi
nzuri zinazoelimisha, kukuza na kuitangaza lugha ya Kiswahili nje ya mipaka ya Tanzania lugha
ambayo imekuwa ikukua kila siku kwa kupitia filamu za kitanzania zinazopenyeza
na kuvuka mipaka ya nchi,” alisema Silondwa.
Alisema kuwa wanaarajia kuwa na Tuzo kubwa zitakazoshirikisha
wadau wote kwa baadae, na kuwa ni moja kati ya moja ya kampuni wadhamini wa
tuzo zenye mlengo wa kimataifa, mwaka huu kampuni imeandaa tuzo hizo pasipo
kuwatumia wadhamini wa nje ya kampuni ikipata udhamini kwa kampuni ya Steps
Solar pekee.
Comments
Post a Comment