STARS NDIO BASI TENA BRAZIL 2014

NDOTO za Tanzania kushiriki fainali za  Kombe la Dunia 2014 nchini Brazil mwaka 2014 zilihitimishwa jana baada ya timu ya Taifa kutandikwa mabao 4-2 dhidi ya Ivory Coast katika mchezo uliopigwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
.Katika mchezo huo ambao Stars waliuanza vizuri,  Amri Kiemba aliiandikia Stars bao la kwanza katika dakia ya kwanza ya mchezo huo 
baada ya kupokea kazi nzuri ya Mbwana Samatta.
Dakika ya 12 Traore Lacina aliisawazishia Ivory Coast akimalizia krosi ya Yaya Toure, kabla ya Yaya kupachika la pili katika dakika ya 23 
na dakika ya 34 Thomas Ulimwengu alisawazisha.
Ivory Coast iliandika bao la tatu katika dakika ya 42 lililofungwa kwa penati na Yaya baada ya beki wa Stars Erasto Nyoni kumsukuma Gervinho ndani ya boksi na kufanya timu hizo kwenda mapumziko kwa Ivory Coast kuongoza kwa mabao 3-2.
Kipindi cha pili kilianza kwa mashambulizi ya kupokezana huku Stars ikishindwa kuzitumia vema nafasi ilizozipata ndani ya kipindi hiyo na hatimaye dakika ya 90  Wilfred Bonny alihitimisha karamu la mabao kwa Ivory Coast kwa kupachikia la nne.