RUVU SHOOTING WANASA NYOTA WA TANZANIA PRISONS

KLABU ya Ruvu Shooting ya Kibaha mkoani Pwani, imefanikiwa kumsajili mshambuliaji Mluga Maguli kwa ajili ya msimu ujao wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

 Muguli alisaini mkataba wa kuichezea Ruvu Shooting mbele ya viongozi wa timu hiyo kwenye ofisi zilizopo 832 KJ, Ruvu JKT, Mlandizi mkoani Pwani.

 Mchezaji huyo ambaye msimu uliopita alikuwa akikipiga Tanzania Prisons ya Mbeya kabla ya kumaliza mkataba wake hivi karibuni.

 Kwa mujibu wa Ofisa Habari wa Shooting, Masau Bwire, usajili wake utakuwa wenye tija na manufaa makubwa, kutoka na uwezo wa hali ya juu aliyonao uwanjani.

 Alisema timu yake itaendelea kusajili wachezaji wenye vipaji na uwezo mkubwa tofauti na klabu nyingine zinazosajili nyota waliochoka.

 Maguli anakuwa mchezaji mpya wa pili kusajiliwa na maafande hao, baada ya mwishoni mwa wiki kumsajili Cosmas Ader aliyekuwa akicheza kwa mkopo African Lyon akitokea Azam Fc.