PIGO TENA TASNIA YA MUZIKI, MSANII LANGA AFARIKI DUNIA

TASNIA ya muziki wa bongo fleva imepata pigo jingine bada ya msanii wa Hip Hop nchini Langa Kileo kufariki dunia.
Langa ambaye alichipukiwa katika shindano la Coca Cola Pop Star kupitia kundi la WAKILISHA akiwa na Sarah Kaisi na Witness Mwijaga alikumbwa na umauti huo jana jioni alipokuwa amelazwa kwenye hospitali ya Taifa ya Muhimbili akisumbuliwa na Malaria.
Kifo cha Langa kinakuja wakati bado tasnia hiyo ikiwa haijapoa machungu ya kuondokewa na mkali mwingine wa muziki huo, Albert Mangwea aliyefariki nchini Afrka ya Kusini mwishoni mwa mwezio uliopita kabla ya kuzikwa kwao Morogoro wiki iliyopita.