MRISHO MPOTO NA MJOMBA BAND KUHAMASISHA KAMPENI YA KUNAWA MIKONO KWA SABUNI NA UJENZI WA VYOO

IMG_1058  
Msanii wa kughani na kuimba nyimbo za asili Mrisho Mpoto ambaye pia ni Mkurugenzi wa ‘Mjomba Band’ akizungumza na Mhariri wa Mo Blog Lemmy Hipolite (kushoto) kuhusiana na kampeni ya kunawa mikono kwa sabuni na ujenzi wa vyoo bora ili kuepukana na maradhi yanayosababishwa na uchafu. Kampeni hiyo itafanyika katika mikoa mitano hapa nchini ikianzia na Dodoma, Mara, Njombe. Rukwa na Tanga.
Na Mo Blog
Mwanamuziki na mghani maarufu wa nyimbo za asili ya nyumbani Mrisho Mpoto amewataka wasanii na wanamuziki wote nchini Tanzania kuwa kitu kimoja kwa kujenga ushirikiano na muungano ili kuweza kuufikisha muziki wa hapa nyumbani katika malengo ya kimataifa.
Akizungumza na Mtandao Maarufu wa Habari jijini Dar es Salaam, Msanii huyo Mrisho Mpoto maarufu kama ‘Mjomba’ amesema katika kujulikana kwenye michezo kama inayofanyika kwa sasa, vikundi vya uhamasishaji vinavyotumia sanaa ya asili ni muhimu kutumika ili kuweza kukuza lugha pamoja na utamaduni wa nyumbani.
Amesema ili kufanikisha usafi wa mazingira ikiwemo siku ya kimataifa ya kunawa mikono ni muhimu jamii ya watanzania kuzingatia usafi ili kuepukana na magonjwa ya kuambukiza yanayotokana na uchafu unaoambukiza maradhi yanayotokana na uchafu.
Aidha amesisitiza jamii kujenga utamaduni wa kujenga na kutumia vyoo bora na kuboresha mzingira kwa ujumla ili kuhakikisha elimu hiyo inawafikia walengwa kwa kubadili tabia na njia mbadala za mawasiliano kuhusu elimu hiyo.
Amesema mwaka 2010 aslimia 9 tu ya wananchi waishio vijijini na asilimia 22 ya wananchi waishio mijini waliweza kupata huduma bora za usafi wa mazingira.
Katika kampeni hiyo Mrisho Mpoto na kundi lake la Mjomba Band wataanzia mikoa ya Dodoma, Mara, Njombe, Rukwa na Tanga kabla ya kuendelea mikoa mingine ambayo kwa pamoja na watashirikianana na Wizara ya Afya na Ustawi wa jamii.