MOYES ATAKA KUMSAJILI BAINES

Klabu ya Everton, imekata ombi lililowasilishwa na Manchester United la kutaka kumsajili mlinda lango wake Leighton Baines kwa kitita cha pauni milioni kumi na mbili.
Kocha mpya wa Manchester David Moyes ambaye alisajiliwa hivi majuzi kutoka kwa klabu hiyo ya Everton alitaka kumasjili mchezaji huyo ili kuimarisha safu yake ya ulinzi.
Siku chache tu baada ya kusajiliwa kama kocha wa Manchester United Moyes, alitangaza wazi wazi kuwa nia yake kuu ni kumsajili mechaji huyo mwenye umri wa miaka ishirini na minane.
Ripoti zinasema Manchester United inajianda kuwasilisha ombi lingine baada ya kuongeza fedha za kumsajili.
Hata hivyo, wasimamizi wa Everton, wamesema kuwa hawana nia yoyote ya kumuuza mchezaji huyo.
Kocha mpya wa Everton, Roberto Martinez kwa upande wake amesema anataka mchezaji huyo ambaye aliteuliwa kuwa mchezaji bora wa mwaka msimu uliopita kusaini mkataba mpya.
Uamuzi huo wa Moyes wa kutaka kumsajili, Baines, huenda ukahujumu nafasi ya mcheza kiungo wa Manchester United Patrice Evra mwenye umri wa miaka thelathini na miwili.
CHANZO:BBC SWAHILI