MISS TABATA 2013 AENDA KUJINOA UJERUMANI

Miss Tabata 2013 Dorice Mollel (22) yupo nchini Ujerumani kwa ziara ya wiki tatu ya kudumisha ushirikiano kati ya nchi hiyo na Tanzania.
Dorice ambaye ni mwanafuzi wa mwaka wa pili katika chuo cha Kumbumbumbu ya Mwalimu Nyerere ni mmoja ya wanafuzi 10 kutoka nchini waliyochaguliwa kwenda mjini Hamburg na Berlin kudumisha ushirikano na kujifunza tamaduni za Kijerumani.
Mratibu wa Miss Tabata, Joseph Kapinga alisema jana jijini Dar es Salaam kuwa ziara hiyo imedhaminiwa na MitOst Hamburg ya Ujerumani na Tanzania Youth Coalition.
“Tunashukuru sana hii ni nafasi pekee kwa Dorice kujifunza mambo mengi kabla ya kushiriki kwenye shindano la Miss Ilala ambayo yamepangwa kufanyika Agosti. Tunaimani ziara hii itapanua mawazo yake na atakuwa tishio kwenye shindano hilo la urembo,” alisema Kapinga.
Dorice ambaye alishinda taji la Miss Tabata Mei 31, aliondoka nchini Juni 6 na atarejea Julai 5.