MISS HIGHER LEARNIG TANZANIA KUANZA KUJINOA IJUMAA @GRAND VILLA HOTEL

WAREMBO wanaotarajiwa kushiriki shindano la Miss Higher Learning 2013 wataanza mazoezi  rasmi Ijumaa ya Juni 21, mazoezi yatakayofanyika kwenye hoteli ya Grand Villa iliyopo Kijitonyama, jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Aggy Classic Entertainment inayoandaa shindano hilo Aggness Mathew alisema kwamba warembo hao watanolewa na mrembo aliyepata kutwaa taji la Kanda hiyo mwaka 2010, Blessing Ngowi (pichani).
 Alisema shindano hilo linatarajiwa kufanyika Julai 5 kwenye ukumbi wa Club Sunsiro ulipo Shekilango jijini Dar es Salaam na kushirikisha warembo 24 kutoka vyuo vikuu vyote vya Tanzania ambapo mwaka huu wamedhamiria kumtoa mshindi wa Miss Tanzania.
 Mratibu huyo aliongeza kuwa, maandalizi mengine kwa ajili ya shindano hilo ambalo taji lake linashikiliwa na Virginia Mokiri kutoka UDOM yanaendelea vema huku akiwaomba wadau na makampuni mbalim,bali kujitokeza kudhamini. 

“Mpaka sasa ni wadhamini wakuu wa Miss Tanzania kinywaji cha Redd’s Original ndio wamethibitisha kudhamini, hivyo tunaomba wadhamini wengine kujitokeza kudhamini shindano letu,”alisema