LIEWIG:SIMBA TUMALIZANE KINDUGU...WAAHIDI KUMLIPA HARAKA IWEZEKANAVYO

WAKATI aliyekuwa kocha wa Simba Mfaransa Patrick Liewig akiutaka uongozi wa timu hiyo kumalizana naye kindugu, uongozi wa timu hiyo umesema kocha huyo ni king'ang'anizi.
Liewig ambaye mkataba wake ulisitishwa mara baada ya kumalizika kwa msimu uliopita wa Ligi Kuu Bara, alitua nchini jana kwa ajili ya kuendelea na kazi kwa madai kwamba hana taarifa za kibarua chake kuota nyasi.
Aidha, Liewig alisema alizungumza na Mwenyekiti wa Simba Ismail Aden Rage ambaye aliahidi kukutana naye kwa mazungumzo mwishoni mwa wiki.
Hata hivyo, Liewig amesema leo kwamba kama Simba haina mpango naye ni bora iachane naye kistaarabu kwani kinyume na hapo wasije kumlamu.
Liewig ameiambia Sports Lady Blog kwamba anataka Simba imlipe mishahara yake ya miezi minne pamoja na fedha zake za kuvunja mkataba.
Akizungumzia hilo, Kaimu Makamu Mwenyekiti wa Simba Joseph Itang'are 'Mzee Kinesi' ameiambia Sports Lady Blog leo kwamba Liewig ni king'ang'anizi kwani anafahamu kibarua chake kusitishwa.
"Huyu kocha ni king'anizi sana kwani kabla hajaondoka tulimpa barua yake...hata hivyo tutamlipa kilicho chake kabla ya kumalizika wiki hii,"alisema Kinesi.po atachukua hatua miezi minne ya mshahara na kuvunjia mkataba, kinesi amemwambia watampa haki zake kabla wk ijayo na wamwambia coach ni mkataba