KOCHA WA YANGA BRANDTS ATUA DAR , KUANZA KAZI KESHO


KOCHA  mkuu wa Yanga Ernie Brandts (pichani) ametua nchini jana usiku na kesho anatarajiwa kuanza kukinoa kikosi hicho kinachojiandaa na michuano ya Kagame.
 Yanga ambao ni mabingwa watetezi wa michuano hiyo, walianza mazozi mapema wiki hii kwenye uwanja wa Shule ya Sekondari Loyola chini ya kocha msaidizi Fred Felix Minziro.