JAPHET KASEBA KUZIDUNDA NA MMALAWI KESHO

Jafet kaseba akitunisha misuli mbele ya Anthony ruta ambaye alikuwa akisimamia zoezi zima la upimaji akisaidiwa na ibrahim kamwe 'bigright' (2)

Bondia jafet kaseba leo amepima tayari kumkabili mpinzani wake Rasco Chimwanza wa malawi katika pambano la ubingwa wa kimataifa.
Zoezi zima la upimaji lilisimamiwa na Anthony ruta,ibrahim kamwe,pendo njau na doctor john lugambila wa muhuimbili na kueleza kuwa mabondia wote wapo katika hali nzuri ya ushindani.
kwa upande wake jafet kaseba amejinadi kumsambaratisha mpinzani wake katika raundi za mapema za mchezo huo.pia kutakuwepo na mapambano ya utangulizi kama juma fundi atazipiga na hasan kiwale (moro best),josef onyango toka kenya atazipiga na seba temba wa morogoro,huku Issa omar-peche boy atakapomvaa bondia mkongwe juma seleman na mapambano mengineyo mengi yatapigwa katika ukumbi huo wa ddc magomeni kondoa 
katika hali ambayo si yakawaida kwa vyama vya ngumi hapa nchini kuwa pamoja kikazi katika mapambano wanayoyasimamia, kwa pambano la jumamosi itakuwa tofauti kwa baadhi ya maofisa wa chini wa vyama vya ngumi kusimamia mapambano kwa pamoja na kuua tofauti zao,na kujirudi kuwa wao ni wamoja katika michezo.