HATIMAYE YANGA YAMSAINI HUSSEIN JAVU, YAMKANA OLOYA

Yanga imemnasa mshambuliaji wa Mtibwa Sugar, Husssein Javu ambaye pia alikuwa akiwaniwa na Simba.

Habari kutoka Yanga zinasema kwamba, nyota huyo amesaini mkataba wa miaka miwili kwa ajili ya kuitumikia klabu hiyo katika michuano mbalimbali itakayoshiriki pamoja na Ligi kuu bara.
Aidha, mabingwa hao wa ligi kuu bara wamekana kumsajili mshambuliaji wa Kimataifa Mganda, Moses Oloya ambaye Simba nayo ilikuwa ikifanya mazungumzo naye