Meneja Uhusiano wa nje wa Vodacom Tanzania, Salum Mwalim
(Katikati) akizungumza na waandishi wa Habari wakati kampuni hiyo ilipotangaza
Zawadi kwa washindi wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania Bara 2012/13. Kampuni hiyo
imetangaza kutumia zaidi ya Tsh Milioni 200 kwa ajili ya zawadi kwa washindi wa
ligi kwa ujumla. Pamoja nae ni Meneja
Uhusiano wa Umma wa Vodacom ,Matina
Nkurlu (Kushoto) na Afisa habari wa TFF. Boniface Wambura.
Mdhamini wa Ligi Kuu
ya soka Tanzana Bara, Kampuni ya Vodacom imetangaza kutumia kiasi cha Shilingi
Mil 200 kwa ajili ya kutoa zawadi ya fedha taslimu katika ligi inayomalizika
mei 18 ambapo sasa Machampioni wa msimu huu watajinyakulia Shilingi Milioni 70.
Mbali ya bingwa, Vodacom pia itatoa fedha kwa timu
inayomaliza nafasi ya pili, ya tatu na
ya nne katika msimamo wa ligi ambazo ni Sh. 35 Milioni, huku Sh. 25 Milioni na Sh. 20 Milioni zote
zikiwa na ongezeko ikilinganishwa na zawadi za fedha zilizotolewa katika msimu
wa 2012 / 2013.
Zawadi hizo zimetangazwa kwa waandishi wa habari jijini Dar
es Salaam na kampuni hiyo kupitia Meneja Uhusiano wa Mambo ya Nje wa Vodacom
Salum Mwalim, ikiwa ni pamoja na kuainisha zawadi za washindi wa mchezaji mmoja
mmoja pamoja na timu iliyoonyesha nidhamu kwa msimu huu.
"Mwaka huu tutatumia kiasi cha Shilingi Milioni 200 kwa
ajili ya zawadi za fedha taslimu kwa
washindi wa Ligi Kuu ya Vodacom huku bingwa akinyakua kitita cha
Shilingi Milioni 70 ikilinganishwa na Sh 50 Milioni za msimu uliopita."
Alisema Mwalim.
Mwalimu amesema lengo la kuongeza zawadi ni matokeo ya
ushirikiano mzuri kati ya wadhamini wa ligi na wadau wengine wa soka na kwa
pamoja kuwa na dhamira ya dhati katika kuendeleza soka nchini.
"Kila mmoja ni shahidi wa namna ambavyo soka letu
limekuwa na namana ambavyo tunakabaliana hatua kwa hatua na changamoto
zinazohusiana na ligi. Ni matumaini yetu kwamba tunapiga hatua na tuna
matumaini ya kufikia kiwango cha juu zaidi cha maendeleo ya soka nchini
yanaonekana." Aliongeza Mwalim
"Kwetu sisi kama wadhamini tutajitahidi kadri
inavyowezekana kuhakiksha tunaleta mabadiliko katika soka la Tanzania,
tunaangalia mpira wa miguu nchini kwa upana zaidi kama mchezo unaopendwa,
unaotuleta pamoja kama taifa na kuitangaza nchi yetu. Falsafa yetu hii
imechangia kwa kiasi kikubwa kuwepo utulivu na ushirikiano mzuri miongoni mwa
wadau na hivyo kutuletea mafanikio." Alisema Mwalim
Zawadi nyingine zilizo tangazwa ni pamoja na zawadi ya
mchezaji bora wa Mwaka golikipa bora, na mfugaji bora kila mmoja anajinyakulia Shilingi Milioni 5.
Aidha, mwamumzi bora na kocha bora kila mmoja atajipatia
Shilingi 7,500,000 kila huku timu iliyoongoza kwa nidhamu itapata zawadi ya
fedha taslimu ya Shilingi Milioni 15.
"Tumekuwa na msimu mzuri uliojaa ushindani na hamasa,
tunatarajia timu zitajipanga zaidi kwa ajili ya msimu ujao na hivyo kuendelea
kuipa ubora ligi yetu."Alisema Mwalim huku akiwashukuru wadau wa mpira wa
miguu nchini ikiwemo Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Bodi ya Ligi, Chama cha
Waamuzi(FRAT), Vilabu, wachezaji na kipekee washabiki na kamati ya ligi kuu.
Amesema bila ya ushirikiano wa wadau hao na wengine ikiwemo
Serikali, ligi kuu ya Vodacom isingeweza kufikia maendeleo iliyoyafikia katika
msimu unaomalizika ambao kwa kiasi kikubwa ulitawaliwa na mpira wa uwanjani na
si vinginevyo.
Comments
Post a Comment