YANGA, COASTAL UNION WAGAWANA POINTI

MANINGWA wa ligi kuu bara, Yanga Sc hii leo wamegawana pointi na Wagosi wa Kaya Coastal Union ya tanga kufuatia sare ya bao 1-1 kwenye mcherzo wao wa ligi hiyo ulipoigwa kwenye uwa wa taifa jijini ar es salaam.
Katika mchezo huo ambao yanga ilichezesha wachezaji wengi wa kikosi cha pili ndiyo ilianza kuandika bao la kwanza dakika ya tatu tu tangu kuanza kwa mchezo kupitia kwa Jerry Tegete aliyeitendea haki pasi ya Nurdin bakari.
Bao hilo lilibadili kidogo hali ya mchezo ambao ulianza kwa taratibu ambapo Abdi Banda aliswazisha klatika dakika ya 16.
Kwa matokeo hayo yanga imefikisha pointi 57 huku Coastal ikiendelea kubaki nafasi ya sita ya msimamo wa ligi hiyo kwa kuwa na pointi 35 nyuma ya Mtibwa Sugar yenye pointi 36 na simba ambayo inashika nafasi ya nne kwa pointi 39, huku nafasi ya tatu ikikaliwa na Kagera Sugar yenye pointi 46 na Azam iliyo ya pili kwa pointi 48.