WINLADY MUSHI NDIYE MISS MOSHI 2013


 Mkurugenzi wa Executive Solution, Aggrey Mareale (wa kwanza kulia, alivaa mavasi meusi),  Mshindi wa pili, Veronica Chami, mshindi wa Redds Miss Moshi, Winlady White (mwenye taji), mshindi wa tatu, Ester Freddy na Mgeni Rasmi, Kamanda wa Polisi ACP-Robert Boaz.picha na Fadhili Athumani.
Washindi wa shindano la Redds Miss Moshi 2013 wakiwa katika picha ya pamoja na waratibu wa mashindano hayo, Kassimu Babi (aliyeshika kipaza sauti) na Mkurugenzi wa New Vision Plan and Company, Moses Komba.picha na Fadhili Athumani.


Na Mwandishi Wetu, Moshi.
WINLADY WHITE MUSHI (20), Mwanafunzi wa mwaka wa pili katikabiashara, Chuo cha Biashara na Ushirika Moshi (MUCCoBS), mshiriki namba 1, ametawazwa kuwa malkia mpya wa urembo Moshi mjini, Redds Miss Moshi 2013.
White mwenye ndoto za kuwa mbunifu wa kimataifa, huku ikiwa ndiomara yake ya kwanza kushiriki ulimbwende, alifanikiwa kutwaa taji hilo na kumrithi Redds Miss Moshi 2012, Angela Filbert.
Timu ya majaji watano wakiongozwa na Jaji mkuu, Jaji Brian walimtawaza Malkia huyo akiwabwaga wapinzani wake, Veronica Chami, Martha Charles, Winnie Macha na Ester Freddy.
sema kwa kuzingatia vigezo vyote vya mashindano ya ulimbwende vinavyotumika kitaifa na kimataifa wote kwa pamoja waliridhika na kila walichokishuhudia kabla ya kuamua kumtangaza Wnlady White kuwa Redds Miss Moshi mwaka 2013.
Washindi wengine ni, Mshindi wa pili, Mshiriki namba 9, Veronica Chami, (1st runner up), mshindi wa Tatu, mshiriki namba 3, Esther Freddy (2nd runner up), mshindi wa 4, mshiriki namba 15, Martha Charles (3rd runner up) huku nafasi ya tano ikienda kwa mshiriki namba 13, Winnie Macha (4th runner up).
Adija Ibrahimu, ambaye ni mshiriki namba 6, alitangazwa kuwa Miss Talent 2013, akimbwaga mpinzani wake wa pekee mshiriki namba 4, Jacky Mushi ambaye tangu mwanzo wa kinyanganyiro alikuwa anapigiwa upatu wa kuchomoka na taji hilo.
Burudani la nguvu liliporomoshwa na Msanii mkongwe wa bongo Fleva, Prince Dully Sykes, akisindikizwa na wasanii wengine kutoka Moshi na kuwakonga mashabiki waliofurika ukumbini hapo akiwemo, mgeni rasmi, Kamanda wa polisi mkoani Kilimanjaro, ACP- Robert Boaz na Mkurugenzi wa Executive Solution, Aggrey Mareale.
Redds Miss Moshi 2013, yaliyofanyika katika ukumbi wa Aventure mjini hapa, yalidhaminiwa na Redds Original, Panone and Company Ltd, Bonite Bottlers, Baba G, A n A Boutique na Zoom net Printers