WASANII MBALIMBALI KUPAMBA MAADHIMISHO YA SIKU YA MAKUMBUSHO YA TAIFA DUNIANI MEI 18



Kaimu mkurugenzi wa makumbusho na nyumba ya utamaduni, Mawazo Ramadhan wa pili kulia akizungumzia maadhimisho ya siku utamaduni duniani, kulia kwake ni mkuu wa idara ya progamu katika makumbusho ya Taira, Irene Mvile, wa tatu kutoka kulia ni Adelaide Sallema ambaye ni mhifadhi mwandamizi na wa kwanza kushoto ni msimamizi wa studio z makumbusho ya Taifa.

WASANII mbalimbali wa sanaa za ufundi wa kazi za mikono na nyinginezo wanatarajiwa kushiriki katika tamasha maalum la siku tatu la  kuadhimisha siku ya makumbusho duniani, linalotarajiwa kuanza mei 16 hadi 18 katika Makumbusho ya Taifa Tanzania yaliyopo mtaa wa Samora  mkabala na Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na waandishi wa habari jana, kaimu Mkurugenzi wa makumbusho ya Taifa,  Mawazo Ramadhan alisema kwamba tamasha hilo litakuwa la wazi huku maadhimisho ya mwaka huu yatabeba kauli mbiu ya Kumbukumbu+ubunifu=mabadiliko katika jamii.
Alisema kupitia maadhimisho hayo pia kutakuwa na uoneshwaji wa video za mambo mbalimbali yaliyotokea kuanzia enzi za kale ambapo kutakuwa pia na maonesho ya  sanaa za aina mbalimbali  yote ikiwa ni katika kuonesha ni jinsi gani kumbukumbu na ubunifu katika kazi zao unavyotumika kuleta mabadiliko katika jamii.
Ramadhan alisema Makumbusho ya Taifa inatoa nafasi kwa wasanii kutumia jukwaa pamoja na viwanja vya maonesho ambapo amewataka wenye nia ya kutaka kushiriki katika kuonesha kazi zao kujitokeza kwa wingi ili kupata fursa pia ya kutangaza kazi zao kupitia maonesho hayo.
“Pia  wadau pamoja na wasaii mbalimbali watajionea kumbi, jukwaa na studio za kisasa ambazo zimeanza kutumika katika makumbusho yetu ambapo wadau watapata fursa ya kujua taratibu mbalimbali za jamii na kupata huduma hizo,”alisema
Siku ya makumbusho duniani ambayo ilianzishwa mwaka 1977 huadhimishwa Mei 18 kila mwaka ambapo siku hiyo itaadhimishwa na Makumbusho zipatazo 32,000 zilizopo nchi 129 duniani kote.

Comments