WASANII KIBAO KUPAMBA TAMASHA LA MASTAA CHIPUKIZI J'2 STARLIGHT HOTEL


Press Release
TAMASHA la Mastaa chipukizi zaidi ya 320 la mwezi Mei litafanyika Jumapili 26, 2013 katika ukumbi wa Starlight Hotel kuanzia saa 4 asubuhi mpaka saa 10 jioni.

Mwenyekiti wa Shiwata, Caasim Taalib alisema maandalizi ya tamasha hilo yamekamilika  na vikundi vya sanaa vya Kaole, Splendid, Super Shine Taarab, Five Star Modern Taarab pamoja na wasanii mbalimbali wa Bongo Flava, Maigizo,Ngoma, Dansi na Sarakasi nao wamethibitisha kushiriki.

Taalib alisema wasanii wakongwe wa bongo flava walioalikwa ni Stara Thomas, Ommy G na waigizaji wakongwe wa Kaole na Splendid wataonesha umahiri wao katika fani ya sanaa Kauli Mbiu ikiwa ni Kilio cha Msanii .

Vikundi vingine vitakaonesha vipaji vyao ni Kepteni  Shaibu, Tanzania Disabled, Uyoga Boga Village, Ndafu Arts Group, CGC, Magengistar Crew, Dodo Arts Group, Culture Arts Group, Wachapa Kazi Academy, Soweto Picture, Shiwata Commedy, Mwavionelachi, Manuari Arts Group, Tandale Morden Taarab na Begeja Wushu,

Wakati huo huo SHIWATA inawapongeza wote walioshiriki tamasha  la Aprili 27 ambako zaidi ya wasanii 300 walishiriki kuonesha vipaji.

 Pia Taalib amelipongeza Shirikisho la Filamu Tanzania (TAFF) kwa ushirikiano wao mzuri na kuwaomba viongozi wengine wa bendi za muziki, taarab,vikundi vya sanaa,mapromota,maprodusa na wadau wote kushiriki katika matamasha haya ili kujenga ushirikiano wa pamoja.


Peter Mwenda 
Ofisa Habari wa SHIWATA
0715/0752-222677


23/5/2013