WAREMBO MISS TABATA WAENDA KUTALII MIKUMI

Washiriki wa Miss Tabata wakiwa katika pozi



Na Mwandishi Wetu
Washiriki wa Dodoma Wine, Redd’s Miss Tabata 2013 usiku wa kuamkia leo waliondoka kwenda kutembelea hifadhi ya taifa ya Mikumi.
Mratibu wa shindano hilo Godfrey Kalinga alisema jana kuwa warembo hao waliondoka na gari ya aina ya Toyota Double Coaster ikiwa na warembo 20 pamoja na walimu na viongozi wao.
Kalinga alisema ziara hiyo ina lengo la kukuza utalii wa ndani na kujenga ushirikiano miongoni mwao.

Alisema kuwa warembo hao pia watapata fursa ya kutembelea vivutio mbalimbali vilivyomo kwenye mbuga hiyo iliyoko mkoani Morogoro.
“Tutarudi Dar es Salaam Jumatatu kujiandaa na shindano letu litakalofanyika Ijumaa ijayo,” alisema Kalinga.
Kadhalika, Kalinga  alisema kuwa ziara hiyo imedhaminiwa na kampuni ya CXC Africa.
 Shindano la kumsaka Miss Tabata  litafanyika Ijumaa ya Mei 31 katika ukumbi wa Da’ West Park, Tabata.
Wadhamini wa shindano hilo ni Nipashe, Redds, Dodoma Wine, Nipashe, Vayle Springs, Multichoice, Fredito Entertainment, Integrated Communications Limited, CXC Africa, Brake Point na Saluti5.
Warembo hao ni Madgalena Bhoke (21), Kabula Juma Kibogoti (20), Upendo Dickson Lema (22), Hidaya David Mwenda (22), Aneth Ndumbalo (19),  Dorice Mollel (22), Eunice Nkoha (19), Kazunde Musa Kitereja (19),  Rehema Kihinja (20),  Pasilida Mandali (21), Brath Chambia (23), Joaniter Kabunga (21), Recho Mushi (20),Caroline Sadiki (20) na  Suzan Daniel (18).
Anayeshikilia taji la Miss Tabata kwa sasa ni Noela Michael ambaye pia ni Miss Ilala.
Miss Tabata inaandaliwa na Bob Entertainment na Keen Arts.

Comments