WAREMBO MISS LINDI 2013 KUINGIA KAMBINI JUMAMOSI @LINDI BEACH RESORT


WAREMBO wanaotarajiwa kushiriki shindano la kumsaka Redd’s Miss Lindi 2013 wanatarajiwa kuingia kambini jumamosi katika hoteli ya Lindi Beach Resort kwa ajili ya maandalizi ya shindano hilo litakalofanyika mwezi ujao.
Mkurugenzi wa kampuni ya Alliance Entertainment  inayoandaa Shindano hilo Shah Ramadhan, alisema kwamba jumla ya warembo 12 wameshathibitisha kushiriki shindano hilo.
Alisema warembo hao kutoka wilaya za mkoa huo wanatarajiwa kunolewa na Miss Pwani 2010, Zainab Mselemu ambapo mwaka huu pia wamejipanga kuhakikisha kuwa watatoa mwakilishi atakayefanya vema kwenye fainali za Miss Tanzania baadaye mwaka huu.
“Kama mjuavyo mkoa wa Lindi una historia ya kufanya vema kwenye fainali za taifa za Miss tanzania kwa miaka tofauti ingawa hatujabahatika kumtoa Miss tanzania lakini tumeweza kufika hadi tatu bora, kutoa wartembo wenye vipaji n.k, hivyo naamini na mwaka huu tutafanya maajabu kwani mwaka jana tu mrembo wetu Irene Veda aliigia 15 bora ya miss Tanzania,”alisema
Shah aliwataja baadhi ya warembo watakaoshiriki shindano hilo ni pamoja na Asha Abdul, Florida daniel, Mwajuma Juma, Sabra Nanji, Pendo Chodasi, Leila Abdul, Angel Kisanga, Zainab Shaban, Sophia Maganga na Janet John.
Aidha, Shah aaliwata wadhamini waliojitokeza mpaka sasa ni pamoja na  Redd's original, Ipinda Trading co. Ltd,Blue View Hotel, Ndanda springs water,Muhsin General enterprises, Live trading Center, Mangroove Bar , Big solution, Mtwara cable television Services, Pride FM Mtwara na  Sports Lady Blog.