TAMASHA LA PILI LA SHIWATA KUFANYIKA MEI 26 STARLIGHT HOTELI


 Press Release
TAMASHA la Mastaa chipukizi la mwezi Mei litafanyika tarehe 26,mwezi huu katika ukumbi wa Starlight Hotel kuanzia saa 4 asubuhi mpaka saa 10 jioni.

Vikundi vya sanaa vya Kaole, Splendid, Super Shine Taarab, Five Star Modern Taarab pamoja na wasanii mbalimbali wa Bongo Flava, Maigizo, Ngoma, Dansi na Sarakasi wamethibitisha kushiriki tamasha hilo.

Wasanii wakongwe wa bongo flava kama Stara Thomas, Bendi ya Msondo Ngoma na waigizaji wakongwe wa Kaole na Splendid wataonesha umahiri wao katika fani ya sanaa.

Kauli Mbiu ni Kilio cha Msanii ambako mpaka sasa vikundi 30 kutoka jiji la Dar es Salaam vitashiriki katika tamasha hilo.

SHIWATA pia inawapongeza wote walioshiriki tamasha  la Aprili 27 ambako zaidi ya wasanii 300 walishiriki kuonesha vipaji vyao ambako mgeni rasmi alikuwa mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM kutoka Wilaya ya Kinondoni, Calist Lyimo ambaye alitumia nafasi hiyo kuwaasa wasanii kujituma kuonesha uwezo wao katika kuelimisha jamii.

Pia Shiwata imeupongeza uongozi wa Shirikisho la Filamu Tanzania (TAFF) kwa ushirikiano wao mzuri na kuwaomba viongozi wengine wa bendi za muziki, taarab,vikundi vya sanaa,mapromota,maprodusa na wadau wote kutoa ushirikiano katika matamasha haya ili kujenga ushirikiano wa pamoja.

Maandalizi ya tamasha hilo yamekamilika ambako wasanii kutoka vikundi mbalimbali wamepiga kambi ya kujifua ili kuonesha ubunifu wao katika tamasha hilo.

Wakati huo huo SHIWATA inatarajia kuhamisha tamasha hilo kwa mwezi Juni kufanyikia mkoa wa Arusha ili kuwapa nafasi wasanii wa mkoa huo nao kuonesha uwezo wao.

Wasanii 100 ambao wamefanya vizuri katika matamasha mawili yaliyokwisha fanyika Dar es Salaam watapatiwa nafasi katika tamasha la Arusha ambalo linafanyika 29/6/2013.

Peter Mwenda 
Ofisa Habari wa SHIWATA
0715/0752-222677

Comments