SOFAPAKA FC KUJA NA JESHI LAKE LOTE KUZIKABILI SIMBA NA YANGA

UONGOZI wa klabu ya Sofapaka ya Kenya umesema kwa 

jinsi wanavyozifahamu timu za Simba na Yanga 

wanaamua kuleta kikosi kizima ili waweze kushinda 

mechi zao zote mbili.

Meneja wa  Sofapaka,  Ngalambe Roberto alisema watatua 

nchini wakiwa na kikosi cha wachezaji 20 na 

viongozi watato ambapo katika kikosi hicho watatua 

na nyota wao wote.

"Sisi tumejiandaa vizuri tunazifahamu na kusoma 

kwenye mitandao kuhusu timu hizi, hivyo tutakuja 

na majeshi yote ili tushinde mechi zote mbili," 

alisema Ngalambe.

Alisema Tanzania kuna timu nyingi nzuri zenye 

ushindani, lakini kwa Simba na Yanga ni zaidi, 

hasa kutokana na upinzani mkubwa uliopo kwa timu 

hizo mbili.

Waratibu wa mechi hiyo Kampuni ya Smartsports 

wameziandalia timu za Yanga na Simba mechi ya 

kirafiki dhidi ya Sofapaka kabla ya timu hizo 

kwenda nchini Sudan kushiriki michuano ya Kombe la 

Kagame.

Mkurugenzi wa Kampuni ya Smartsports George 
Wakuganda alisema baada ya Sofapaka kuwasili 

jijini Dar es Salaam, itacheza mechi yake ya 

kwanza Juni 12 dhidi ya Simba, itakayopigwa kwenye 

Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Alisema Juni 13, kikosi hicho kutoka Kenya 

kitashuka tena uwanjani kuumana na mabingwa wa 

Ligi Kuu Tanzania Bara na Afrika Mashariki (Kombe 

la Kagame), Yanga.

Alisema mechi hiyo itakuwa nafasi nzuri kwa 

mashabiki wa timu hiyo kuwaona wachezaji wao wapya 

waliosajili kwa ajili ya msimu ujao, Mrisho Ngassa 

na Amri Kiemba, kwa mara nyingine tena wakivaa 

jezi za rangi ya njano na kijani.

Yanga hivi karibuni imewatangaza wachezaji wapya 

wawili, wakitokea Simba, huku Haruna Niyonzima 

akiongeza mkataba wa miaka miwili wa kuitumikia 

timu hiyo
.

Comments