SIMBA YACHUMPA NAFASI YA TATU YA VPL

WEKUNDU wa Msimbazi Simba Sc wamejikusanyia pointi tatu jioni ya leo baada ya kuwabanjua maafande wa Ruvu Shooting kwa mabao 3-1, katika mchezo wa ligi kuu Bara uliopigwa kwenye uwanja wa taifa jijini dar es Salaam.
Ushindi huo umeifanya Simba ifikishe pointi 42 na hivyo kupanda kutoka nafasi ya nne hadi ya tatu ya msimamo wa ligi hiyo inayoongozwa na Yanga ambao tayari wameshatwaa ubingwa wakiwa na pointi 57, huku Azam Fc ikiwa ya pili kwa pointi 48.
Katika mchezo wa leo Simba pamoja na ushindi huo Simba watajilaumu sana baada ya nyota wake kukoisa mabao mengi ya wazi.
Alikuwa Amri Kiemba aliyeanza kuifungia Simba bao la kwanza katika dakika ya 14, bao ambalo lilibadilisha hali ya mchezo na timu kuanza kushambuliana.
Hata hivyo timu hizo zilikwenda mapumziko kwa Simba kuongoza kwa bao 1-0.
kipindi cha pili kilianza kwa taratibu ambapo mabadiliko kwa kila timu yaliweza kuingeza ushindani huku wachezaji wakichezeana rafu za hapa na pale.
Mwamuzi wa mchezo aliwazawadia kadi za njano kwa sababu tofauti,Mrisho Ngassa wa Simba, Said Madega na Ernest ernest wa Ruvu Shooting.
Katika mchezo huo anmbao Simba ilipambwa na wachezaji chipukizi zaidi, Edward Christopher aliiandikia bao la pili kabla ya Ismail Mkoko kuandika la tatu dakika mbili baadaye. 
Katika mchezo wa leo, Simba iliwatoa Haruna Chanongo, Felix Sunzu na Ramadhan Singano na kuwaingiza Ismail Mkoko, Mrisho Ngassa na Edward Christopher, huku Shooting iliwatoa Said Dilunga, Said madega na Rafael Kagalu na kuwaingiza Kulwa Mfaume, Hamis Kisuke na Ayoub Kitale.