SIMBA WAIONYA YANGA KUHUSU NGASSA

SAA chache kabla ya kufanyika kwa mechi ya watani wa jadi nchini Simba na Yanga, uongozi wa Simba umewaonya mahasimu wao Yanga kuacha kumvuruga kisaikolojia nyota wa timu hiyo Mrisho Ngassa.
Simbva na Yanga zitakwaana kesho kwenye dimba la Taifa jijini Dar es Salaam katika moja ya mchezo wa funga dimba la Ligi Kuu bara itakayohitimishwa kesho kwa viwanja sita vingine pia nyasi zake kuwaka moto.
Simba imeamua kuitolea uvivu Yanga baada ya kukithiri kwa taarifa kuwa itamtambulisha Ngassa rasmi  kama mchezaji wa timu hiyo mara baada ya mchezo wa kesho.
Ofisa habari wa Simba, Ezekiel Kamwaga amesema leo kwamba,taarifa zinazotolewa na Yanga juu ya mchezaji huyo zimelenga kumvuruga kisaikolojia ili ashindwe kuitumikia vema timu yake hapo keshop.
"Kwa kweli ni taarifa za kumvuiruga kisaikolojias mchezaji wetui na hasa ikizingatiwa kuwa mchezo wa kesho unahitaji mchezaji kuwa sawa kisaikoloji lakini kwa Yanga wanavyofanya sio uuungwana kwani itapelekea mchezaji ashindwe kjutimiza wajibu wake uwanjani,"alisema.
Kamwaga aliongeza kuwa mbuinu wanazozitumia Yanga kuidhoofiosha Simba katika mchezo wa kesho zimepitwa na wakati hivyo hawana budu kuelekeza akili zao katika maandalizi ya mchezo na si kutaka kuwavuruga wachezaji wa Simba.
Akizungumzia mchezo wa kesho, Kamwaga alisema kikosi kipo tayari kwa mchezo huo na wachezaji wamepania kufuta machozi ya kuukosa ubingwa kwa kushinda mechi ya kesho.
Tayari Yangas imeshatwaa ubingwa wa ligi hiyo mapema, huku mchezo wa keshji ukitarajiwa kuwa na ushindani mkubwa ambapo kila timu imetamba kuibukas nas ushindio.
katika mchezo wa mzunguko wa kwanza, timu hizo zilitoka sare ya bao 1-1.