SIMBA KUSIMAMA DAKIKA MOJA KESHO KUMUOMBEA MAFISANGO

WAKATI leo umetimia mwaka mmoja tangu kufariki kwa kiungo wa kimataifa wa Simba Mnyarwanda Patrick Mafisango (pichani), wachezaji, mashabiki na viongozi wa vklabu hiyo kesho watasimama kwa dakika moja kwa ajili ya kumuombea dua nyota huyo.
Mafisango alikutwa na umauti alfajiri ya Mei 17 katika eneo la Veta, Chang'ombe jijini Dar es Salaam kwa ajali ya gari.
Ofisha habari wa Simba, Ezekiel Kamwaga amesema leo kwamba katika kumuenzi nyota huyo kesho kabla ya kuanza kwa mechi yao na Watani wao wa jadi nchini Yanga itaskayopigwa kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam watasimama kwa dakika moja kwa ajili ya kuomboleza.
Alisema hawana budi kufanya hivyo kutokana na mchango mkubwa alioutoa mchezaji huyto ndani ya klabu hiyo ikiwemo kuiwezesha kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu soka Tanzania Bara mwaka 2011/2013.
RIP Patrick Mutesa Mafisango