RAIS wa Heshima wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) Alhaj
Muhidin Ndolanga amelipongeza Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA) kwa
kubatilisha mchakato wa uchaguzi wa viongozi wa TFF na kuagiza zoezi kufanyika
upya.
Fifa ilifikia uamuzi huo kufuatia kuwepo baada ya kubaini kasoro iliyotokana na ukosefu
wa kutokuwepo vyombo vya kushughulikia ukiukwaji wa maadili.
FIFA ambayo ilituma ujumbe wake katikati ya mwezi uliopita
kufanya utafiti kuhusu mchakato wa Uchaguzi Mkuu wa TFF ambao ulisimamishwa
baada ya baadhi ya wagombea kulalamika, imetaka uchaguzi ufanyike kabla ya
tarehe 30 Oktoba 2013, lakini ukitanguliwa na mabadiliko ya katiba ambayo
yatahusisha uundwaji wa vyombo vya kushughulikia ukiukwaji wa maadkwa utata wa
zoezi hilo uliotokana na kuenguliwa kwa baadhi ya wagombea bila ya sababu za
msingi, huku pia mchakato huo ukiendeshwa kwa katiba batili.
Akizungumza kwenye kipindi cha Spoti leo kinachorushwa na
Redio One juzi, Ndolanga alisema hadhani TFF kama itavurunda tena zoezi hilo
kama ilivyokuwa awali.
Ndolanga ambaye alikuwa ni mmoja ya wadau waliohojiwa na
Fifa juu ya utata wa uchaguzi huo alisema kwamba, anaamini TFF itajipanga
vizuri katika hilo ili haki iweze kutendeka kwa kila mmoja.
“Sidhani kama hivi sasa tutaendeleza matatizo ya awali,
Katiba ilivunjwa na kubadilishwa kwa waraka hivyo naamini itarekebishwa kwa
mujibu wa taratibu na kisha tuendelee na taratibu nyingine.
Aidha, Ndolanga alitoa rai kwa wajumbe wa mkutano mkuu kuwa
makini katika zoezi la kubadilishwa kwa katiba ya TFF kwa kuhakikisha wanaingiza vitu ambavyo
vitaleta faida kwa Taifa zima la Tanzania.
Comments
Post a Comment