MWILI WA NGWAIR WAANZA KUFANYIWA UCHUNGUZI NCHINI AFRIKA KUSINI, SWAHIBA WAKE NAE ALAZWA ICU

MWILI  wa msanii wa bongo fleva Albert Mangwea 'Ngwair' umehamishwa kutoka hospitali ya Hellen Joseph na kupelekwa katika mochwari ya Taifa nchini Afrika Kusini kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi.
Mkali huyo wa mitindo huru 'Free styles' alikutwa na umauti nchini humo jana katika gheto la rafiki yake akiwa usingizini.
Taarifa kutoka nchini afrika kusini zinasema kwamba mwili huo utafanyiwa uchunguzi ili kubaini chanzo cha kifo cha msanii huyo  kabla ya taratibu za kuusafirisha kuja nchini kwa mazishi kuendelea.
Habari zisizo rasmi pia zinaeleza kuwa chanzo cha kifo cha msanii huyo ni kutokana kutumia dawa za kulevya kwa kiasi kikubwa.
Katika hatua nyingne, msanii mwingine wa bongo fleva ambaye pia aloikuwa nchini humo anayefahamika kwa jina la M2 the P naye amelazwa katika chumba cha uangalizi maalum 'ICU' katika hospitali hiyo ya Hellen joseph.