MSANII MANGWEA AFARIKI AKIWA AFRKA KUSINI

HABARI za kusikitisha zilizopatikana jioni ya leo ni kwamba msanii wa muziki wa bongo fleva, albert Mangwair maarufu kam,a ;ngwair' amefariki dunia akiwa nchini Afrika kusini.
Hata hivyo, taarifa kutoka ofisi za ubalozi wa Tanzania nchini huko zinaeleza kwamba bado hawajapata taarifa rasmi zaidi ya kusikia juu juu tu.
Mangwair ambaye anadaiwa alikuwa huko kwa ajili ya shughuli za kimuziki, alifia kwenye hoteli moja baada ya kutoiamka tangu alipolala usiku wa jana.
Taarifa hizo zisizo rasmi zinaeleza kwamba, nyota huyo alizidisha kiwango cha dawa za kulevya ambacho ndio chanzo cha kifo chake.
Kifo cha ngwair ambaye alikuwa ni muasisi wa kundi la Chamber squad la jijini Dar es salaam, kimeleta simanzi kubwa kwa wadau wa muziki huo.
Ngwai ambaye alikuwa na kipaji cha pekee cha kuimba kwa mtindo huru 'free styles' alipata kutamba na nyimbo kama GHETO LANGU, HOSTEL, MIKASI, SPEED 120, TUPO JUU N.K.
msiba wa msanii huyo upo nyumbani kwa mama yake huko Kihonda njia ya kuelekea Mazimbu mjini Morogoro huku familia nayo ikigubikwa na utata juu ya taarifa za kifo hicho.
RIP