LUNDENGA ATEMBELEA KAMBI YA MISS KIGAMBONI

 Mkurungenzi wa Miss Tanzania Hashim Lundenga akizungumza na warembo wanaowania taji la Miss Kigamboni alipotembelea kamabi yao iliyopo ukumbi wa Break Point katikati ya jiji la Dar es Salaam.Shindano la hilo linatarajiwa kufanyika Juni 7 kwenye Ukumbi wa Navy Beach, Kigamboni jijini Dar es Salaam.
 Baadhi ya warembo wanaowania taji la Miss Kigamboni wakisikiliza maelezo kutoka kwa Kamati ya Miss Tanzania (Hawapo pichani) walipotembelea katika kambi yao ya mazoezi.
 Lundenga akizungumza na warembo wa Miss Kigamboni (Hawapo Pichani) kushoto kwake ni Katibu wa Kamati ya Miss Tanzania Bosco Majaliwa na wa kwanza kushoto ni ofisa habari wa Miss tanzania, Hidan Ricco.
Washiriki wa Miss Kigamboni wakiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi wa Kamati ya Miss Tanzania.