KIPA WA SIMBA APEWA UNAHODHA UGANDA CRANES

KAMPALA, Uganda

KIPA wa timu ya Simba ya Tanzania, Abel Dhaira amepewa unahodha wa timu ya taifa ya Uganda, Uganda Cranes kuelekea mechi ya kirafiki ya kimataifa dhidi ya Libya itakayopigwa kesho.
Uteuzi wa kipa huyo mwenye umri wa miaka 25, umefanywa na kocha mpya, Milutin 'Micho' Sredojevic, akimweka kando nahodha wa muda mrefu, Hassan Wasswa.
Wasswa ndie aliiongoza timu hiyo kutwaa ubingwa wa Kombe la Cecafa, mara zote amekuwa akiokewa jukumu hilo na Andy Mwesigwa, Denis Onyango na Simeone Masaba.
Uteuzi Dhaira, ni wazi atakuwa kipa wa kikosi cha kwanza badala
ya Onyango anayecheza soka ya kulipwa  katika timu ya Mamelodi Sundowns.
Uganda na Libya zimepanga kutumia mechi hiyo kama kipimo kuelekea kampeni ya kusaka tiketi ya fainali za Kombe la Dunia zitakazochezwa mwakni nchini Brazil.
Wakati Uganda inakabiliwa na mechi dhidi ya Liberia wapinzani wao Libya, watakumbana na DR Congo kwenye mechi itakayopigwa Juni 8.