JUMA KASEJA ATOA MASHARTI ILI KUBAKI SIMBA SC


Nahodha wa timu ya Simba, Juma Kaseja ameweka sharti la kupatiwa kitita cha dola 40,000 (sh mil 64) ili asaini mkataba mpya.
Kaseja ambaye pia ni kipa namba moja wa timu hiyo aliyeitumia zaidi ya miaka 10, mkatabata wake unamalizika mwezi huu.
Habari kutoka ndani ya klabu ya Simba zinasema kwamba, nyota huyo ametaka kiasi hicho cha fedha ili aweze kuongeza mkataba mwingine wa kuitumikia klabu lakini haitawezekana kwani ni dau kubwa.
Kiongozi mmoja wa Simba ambaye hakupenda kutajwa jina lake, alidokeza jana, ingawa bado wanamhitaji kipa huyo, kiasi anachotaka ni kikubwa.

“Kweli bado tunamuhitaji Kaseja, lakini kwa hali iliyopo hatuna kiasi hicho cha fedha. Ngoja tusubiri amalize majukumu yake ya kuitumikia timu ya Taifa halafu tutakaa naye na kuzungumza,”alisema.
Hata hivyo, taarifa kutoka kwa mtu wa karibu wa Kaseja zinaeleza, hata kama uongozi utaafikiana naye kuhusiana na mkataba wake, kuna mambo anataka yawekwe sawa.
Moja ya mastarti hayo ni kuhakikishiwa kwa nafasi yake ndani ya klabu hiyo, pamoja na uongozi kutoingilia benchi la ufundi.
“Unajua Kaseja ameona kuna mambo kadhaa ya kuzungumza na uongozi kwanza ili yaweze kumlinda katika mkataba wake,”alisema
Kaseja ambaye alikuwa tishio katika miaka ya nyuma kiasi cha kupachikwa jina la ‘Tanzania One’ katika siku za hivi karibuni kiwango chake kimeonekana kushuka.
Baada ya kuona hali hiyo, uongozi wa Simba katika dirisha dogo la usajili ilimsajili kipa