DRFA YAZIWEZESHA ABAJALO, RED COAST & FRIENDS RANGERS



Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA), Almas Kassongo (kushoto), akimkabidhi  Mwenyekiti wa Red Coast,  Jumanne Ayubu Sh 700, 000 ikiwa ni mchango wa chama hicho kusaidia timu hiyo katika Ligi ya Mabingwa inayotarajiwa kuanza Mei 12 mwaka huu



CHAMA Cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA), kimezizawadia timu zake tatu za Red Coast, Abajalo na Friends Rangers zilizofanikiwa kucheza Ligi ya Mabingwa inayotarajiwa kuanza Mei 12 mwaka huu.

Makabidhiano hayo yalifanyika jana Alhmaisi (Mei 9) jioni kwenye ofisi za chama hicho, zilizopo makutano ya mtaa wa Mafia na Bonde, ambapo Red Coast waliokuwa washindi wa kwanza walikabidhiwa Sh 700, 000, huku Abajalo wao wakizawadiwa Sh 600, 000 na Friends Rangers wakijipatia Sh 500, 000.

Kwa mujibu wa Ofisa Habari wa DRFA, Mohamed Mharizo, lengo la timu hizo kukabidhiwa fedha hizo Viongozi waliohudhuria makabidhiano hayo kutoka DRFA ni Mkurugenzi wa Ufundi, Joseph Kanakamfumo, Afisa Tawala, Said Pambalelo,  Mjumbe wa Kamati ya Ufundi na Mashindano, Daudi Kanuti na Mweka Hazina Ally Hassani.

Wawakilishi wa timu ni Mwenyekiti wa Red Coast, Jumanne Ayubu, Meneja wa Friends Rangers, Shaaban Marsila na Mjumbe wa Kamati ya Utendaji wa Abajalo, Abbasi Ngau.

Wakati huo huo, kamati ya ufundi ya DRFA kesho Jumamosi Harbours Club Kurasini, itakutana na Viongozi wa soka la Wanawake (TWFA), Viongozi wa soka la Vijana na Kamati ya Waamuzi ili kupanga utaratibu wa ligi na pia kuandaa kozi ya makocha.




Comments