BASATA LAOMBOLEZA KIFO CHA MANGWAIR, MWILI WAKE KUWASILI KESHO


Baraza la Sanaa la Taifa limepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za msiba wa msanii wa tasnia ya Muziki nchini Albert Mangwea a.k.a Ngwair.
“ Baraza limestushwa na kuhuzunishwa sana kutokana na taarifa ya kifo hiki cha Ngwair ambaye mchango wake unahitajika sana katika tasnia ya sanaa, pengo aliloliacha ni kubwa kwani ubunifu wao bado unahitajika katika tasnia hii.” Baraza linatoa pole kwa familia ya marehemu na wasanii wote nchini, aidha linawatakia moyo wa subira katika wakati huu wa majonzi ya kuondokewa na mpendwa wetu.
Tunaomba mwenyezi Mungu aipumzishe mahala pema peponi roho ya marehemu. Baraza liko pamoja na familia ya marehemu katika kipindi hiki kigumu cha maombolezo, tutambue kuwa haya ni mapenzi ya Mungu.

Imetolewa na
Ghonche materego
Katibu Mtendaji
Baraza la Sanaa la taifa.

Katika hatua nyingine, mwili wa marehemu Mangwair unatarajiwa kuwasili nchini kesho kutoka Afrika Kusini kabla ya Jumapili kuagwa kwenye viwanja vya Leaders, Kinondoni jijini Dar es Salaam na baadaye kusafirishwa nyumbani kwao Kihonda, Morogoro ambapo mazishi yatafanyika Juni 3 mwaka huu.