BARAZA LA WAZEE YANGA LAMHADHARISHA MWAMUZI WA MECHI YA WATANI


Katibu Mkuu wa Baraza la Wazee wa klabu ya Yanga mzee Ibrahim Akilamli (katikati) akiongea na wandishi wa habari makao makuu ya klabu leo
Kuelekea mchezo dhidi ya Simba SC mei 18, Baraza wa wazee wa klabu ya Young Africans limeomba mwamuzi wa mchezo huo achezeshe kwa kufuata sheria 17 zote za mchezo na kwa kufanya hivyo mabingwa wapya wa Ligi Kuu ya Vodacom watoto wa Jangwani lazima wataibuka na ushindi katika mchezo huo.
Akiongea na wandishi wa habari kwa niaba ya baraza la wazee makao makuu ya klabu, katibu mkuu wa baraza la wazee Mzee Ibrahim Akilimali (Ibrahimovich) amesema wanaamini kikosi cha Yangaa kitaibuka na ushindi katika mchezo huo ikiwa mwamuzi atachezesha kwa kufuata sheria zote 17 na kanuni za soka.
Akilimali amesema Yanga ni timu bora kwa sasa katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kati kila mmoja anajua hilo, tuna wachezaji wazuri wenye kiwango cha hali ya juu ambao wamepikwa wakapikika wakaiva matunda ya mafunzo yao ndio yaliyotupatia ubingwa kabla ya ligi kumalizika.
Aidha aliongeza kuwa "Tunaahidi kwamba tutamfunga Simba SC siku ya mei 18 kutokana na umoja wetu, mshikamano na uongozi bora chini ya mwenyekiti Yusuf Manji na makamu wake Clement Sanga ambao mpaka sasa wameifnaya timu ya Yanga kuwa ya kuogopewa ukanda wote huuu".
Naye Mzee Hashim Mwika aliongeza kuwa waanahidi ushindi katika mchezo huo, idadi ya mabao haijalishi lakini kikubwa tunasema lazima tumfunge Simba mei 18 kikubwa tunaomba mwamuzi achezeshe kwa kufuata kanuni 17, na kama wakifanya hivyo basi Simba Sc wajiandae kupokea mvua ya mawe siku hiyo.
"Mwaka jana walitufunga kwa sababu hatukuwa pamoja, hatukua na maelewano lakini hivi sasa Yanga ni moja kuanzia viongozi, wachezaji, makocha na wanachama hivyo tunamini kwa kuwa pamoja na timu yetu bora lazima simba achezee kichapo "alisema mzee Mwika.
chanzo:www.youngafricans.co.tz

Comments