AFISA UTAMADUNI MKOA WA TANGA ATEMBELEA KAMBI YA MISS UTALII ILIYOPO MKOANI HUMO


Afisa Utamaduni Jiji la Tanga, Peter Semfuko (katikati) ,Matron Hilda Mwinyi (Kulia), na Mratibu wa kamati ya maandalizi Kessy Salum Mbasha (Kushoto) wakiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa fainali za taifa za Miss Utalii Tanzania 2013, alipo kwenda kukagua kambi na kuzungumza na warembo hao Jana katika hoteli ya Mwambani Tanga Beach.

Wakati Maandalizi ya fainali za taifa za Miss Utalii Tanzania 2013 yanaendelea kwa kasi katika hoteli ya kitalii ya Mwambani iliyopo katika ufukwe wa Tanga, huku kila Mrembo akijifua vikali, Afisa Utamaduni wa Mkoa wa Tanga Ndugu Peter Semfukwe ametembelea kambini hapo, kujionea yeye mwenyewe warembo wa Miss Utalii Tanzania 2013 ambao wanajiandaa na Fainali hizo za Taifa zitakazo fanyika wiki Ijayo,kasha alizungumza nao na kuwakaribisha mkoani Tanga.
Afisa Utamaduni  alisema  kuwa amefurahi kukutana na warembo wote wakiwa katika Afya Njema, Mvuto na kila mmoja kuonekana ndiye atakaye twaa taji hilo la Miss Utalii Tanzania 2013, pia ameipongeza kamati ya maandalizi kwa juhudi na jitihada kubwa za kuandaa mashindano hayo ambayo dhima yake ni kuutangaza utalii wa ndani pamoja na utamaduni wa Mtanzania.  Aliongeza kuwa anaahidi  ushirikiano mkubwa wa hali na mali wakati wa maandalizi mpaka mwisho wa mashindano hayo.
Akizungumza na Warembo wa Miss Utalii Tanzania 2013 pamoja na Kamati ya Maandalizi ya Miss Utalii Tanzania , Afisa Utamaduni aliwaasa warembo hao wawe na heshima, adabu, na pia wawe ni mfano bora wa kuigwa katika jamii ikiwa ni warembo hao kuwa mstari wa mbele katika kushiriki, kutangaza Utalii na Utamaduni wa Mtanzania.
Mpaka sasa Kambi ya Miss Utalii Tanzania 2013 ipo jijini Tanga Mwambani Hotel na inaendelea Vizuri, Warembo zaidi ya 30 kutoka mikoa yote nchini ,wanajiandaa vizuri  kwa ajili ya Fainali Hizo zitakazo fanyika wiki ijayo Tanga, Kanda Maalum ya Zanzibar na Vyuo vikuu Tanzania.
Akizungumzia, juu ya maendeleo ya kambi, Fredy Njeje, alisema kuwa baada ya kukwamishwa na wadhamini walio toa ahadi hewa, wamelazimika kuhamishia shindano hilo mkoani Tanga,baada ya kuvutiwa na mwamko wa wafanya biashara na makampuni ya Jiji la Tanga wa kuwa na uwezo wa kudhamini matukio makubwa ya kitaifa na kimataifa.
Tunakabiliwa na changamoto ya warembo wengi kuwa wapya katika kambi yetu,baada ya wale waliokuwako kambini kabla ya kambi kuahirishwa kushindwa kurudi kambini kwa sababu mbalimbali,zikiwemo za kimasomo na wengine kukata tama baada ya kuahirisha. Hata hivyo tayali nafsi zao zimechukuliwa na washindi wa pili wa mikoa yote ambayo warembo wake wameshindwa kurudi kambini, na tayali warembo 30 wameripoti kambini na tunategemea wengine 10 kuripoti kambini wakati wowote ili kufikisha idadi ya warembo 40 wata kao panda jukwaani. Tumejiandaa na tunapata ushirikiano mkubwa kwa serikali ya mkoa nay a Jiji la Tanga, hivyo kutuhakikishia kuwa tarehe itakayo pangwa sasa haitabadilika tena wala kuahirishwa. Tarehe kamili ya shindano itatangazwa kesho na mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ambaye pia ni Afisa Utamaduni wa Jiji la Tanga.
Washindi wa 1-5 wa Fainali za Taifa ,watawakilisha Tanzania katika mashindano mbalimbali ya Dunia na nchi yatakako fanyika katika mabano  International Miss Tourism World (Marekani), Miss Tourism United Nation (Mexico), Miss Heritage World (Tunasubiri Taarifa), Miss Tourism University World(Tanzania), Miss Globe International (Uturuki), Miss Tourism World ( Equatorial Guinea ), Miss Freedom Of The World ( Kosovo) , na Miss Tourism United Nation (Nigeria)  n.k

Wakati huohuo, katika kuhakikisha kuwa maandalizi ya Fainali za taifa, za mashindano hayo ambapo mkoa wa Tanga unakuwa wenyeji kwa mara ya kwanza yanafanyika kwa ubora na hayakwami, kamati ya maandalizi ya kimkoa umeundwa ambayo mwenyekiti wake ni Peter Semfuko Afisa Utamaduni wa Jiji la Tanga. Miss Utalii Tanzania ,hadi sasa tunashikilia Jumla ya mataji 5 ya Dunia na kimataifa, yakiwemo ya Miss Tourism World 2005-Africa,Miss Tourism World 2006-SADC,Miss Tourism World 2007-Africa, Miss Tourism
Model Of The World 2008-Personality, Miss Africa 2006 – 1ST Runner Up n.k

Asante,
 Fredy Njeje
Mkurugenzi wa Masoko na Mahusiano ya Umma


Comments