ABDALLAH KIBADEN AANZA KAZI SIMBA SC

KOCHA mpya wa Simba Abdallah 'king' kibaden kesho anatarajiwa kuana kukinoa rasmi kikosi cha timu hiyo kwa ajili ya kujiandaa na michuano ya kombe la Kagame itakayofanyika mwezi ujao nchini Sudan.
Kibaden ambaye awali alikuwa akiinoa klabu ya kagera Sugar kabla ya kutua Simba na kurithi mikoba ya Mfaransa Patrick liewig, leo alihidhuria mazoezi ya baadhi ya wachezaji wanawania kusajiliwa na klabu hiyo yaliyofanyika katika uwanja wa jkines chini ya kocha msaidizi, jamhuri kihwelo 'julio' na kocha wa vijana, suleiman matola.
ofisa habari wa simba, ezekiel kamwaga amesema leo kwamba Kibaden kesho ataanza rasmi programu yake hiyo kwenye uwanja wa kinesi ambapo wacvhezaji wote waliosajiliwa na Simba wanatakiwa kufika.