WAREMBO 16 WATEMWA SHINDANO LA MISS TABATA 2013


Na Mwandishi Wetu
Jumla ya warembo 16 wametemwa katika kinyang’anyiro cha kumtafuta Redds Miss Tabata ambao utafanyika Mei 31 Dar West Park.
Mratibu wa shindano hilo, Godfrey Kalinga, alisema jana kuwa warembo hao wametemwa kutokana na sababu mbali mbali ikiwemo utoro, kukosa sifa za kushiriki na utovu wa nidhamu.
Kalinga aliwataja warembo waliyotemwa kuwa ni Sophia Claud (21), Lilian Mpakani (19), Lilian Msanchu (19), Rita Frank (20), Pasilida Mandali (21), Rachel Mussa (19), Jasmin Damian (18), Angelina Mkinga (19), Mercy Mwakasungu (20), Tunu Hamis (19), Ray Issa (22), Shamim Abass (22), Shan Abass (22), Amina Ally (18), Magdalena Bhoke (21)  na Zilpha Christopher (19)
Kalinga aliwataja warembo wanoendelea na mazoezi katika umbumbi wa Dar West Park, Tabata kila siku kuwa ni Hidaya David (22), Aneth Ndumbalo (19), Dorice Mollel (22), Eunice Nkoha (19), Kazunde Kitereja (19),  Angela Fradius (19), Domina Soka (21), Rehema Kihinja (20) and  Glory Jigge (18).
Wengine ni Rachel Mushi (20), Caroline Sadiki (20), Kabula Juma Kibogoti (20), Blath Chambia (23), Suzzane Daniel Gingo (18), Upendo Lema (22), Pasilida Mandari (21) na Martha Gewe (19).
Washindi watano kutoka Tabata watafuzu kushiriki Redds Miss Ilala baadaye mwaka huu.
Anayeshikilia taji la Miss Tabata ni Noela Michael ambaye pia ni Miss Ilala.
Redds Miss Tabata inaandaliwa na  Bob Entertainment na Keen Arts na chini ya Udhamini wa Redds, CXC Africa, Fredito Entertainment, Brake Points na Saluti5.